Romans 14

1Mpokeeni yeyote ambaye ni dhaifu katika imani, bila kutoa hukumu kuhusu mawazo yake. 2Mtu mmoja ana imani ya kula chochote, mwingine ambaye ni dhaifu anakula mboga tu.

3Mtu ambaye anakula kila kitu asimdharau yeye asiyekula kila kitu. Na yeye ambaye hali kila kitu asimuhukumu mwingine ambaye hula kila kitu. Kwa kuwa Mungu amekwisha mpokea. 4Wewe ni nani, wewe ambaye unamuhukumu mtumishi ambaye ni miliki ya mtu mwingine? Ni mbele ya Bwana wake kwamba husimama au huanguka. Lakini atainuliwa, kwa kuwa Bwana anaweza kumfanya asimame.

5Mtu mmoja huthamini siku moja kuliko nyingine. Mwingine huthamini kila siku sawa sawa. Hebu kila mtu na ashawishike katika akili yake mwenyewe. 6Yeye ambaye anashika siku, anashika kwa ajili ya Bwana. Na kwa yeye alaye, hula kwa ajili ya Bwana, kwa kuwa anampa Mungu shukrani. Yeye ambaye hali, hujizuia kutokula kwa ajili ya Bwana. Yeye pia hutoa shukrani kwa Mungu.

7Kwa kuwa hakuna aishie kwa nafsi yake, na hakuna afae kwa ajili yake mwenyewe. 8Kwa kuwa ikiwa tunaishi, tunaishi kwa ajili ya Bwana. Na ikiwa tunakufa, tunakufa kwa ajili ya Bwana. Basi ikiwa tunaishi au tunakufa tu mali ya Bwana. 9Kwa kuwa ni kwa kusudi hili Kristo alikufa na kuishi tena, kwamba awe Bwana wa wote wafu na waishio.

10Lakini wewe, kwa nini unamuhukumu ndugu yako? Na wewe, kwa nini unamdharau ndugu yako? Kwa kuwa sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu. 11Kwa kuwa imeandikwa, “Kama niishivyo,” asema Bwana, “Kwangu mimi kila goti litapigwa, na kila ulimi utatoa sifa kwa Mungu.”

12Hivyo basi, kila mmoja wetu atatoa hesabu yake mwenyewe kwa Mungu. 13Kwa hiyo, tusiendelee tena kuhukumiana, lakini badala yake amua hivi, kwamba hakuna atakaye weka kikwazo au mtego kwa ndugu yake.

14Ninajua na nimeshawishika katika Bwana Yesu, kwamba hakuna kitu kilicho najisi chenyewe. Ni kwa yeye tu anayedhani kuwa chochote ni najisi, kwa kuwa kwake ni najisi. 15Ikiwa kwa sababu ya chakula ndugu yako anahuzunika, hautembei tena katika upendo. Usimharibu kwa chakula chako mtu ambaye kwa ajili yake Kristo alikufa.

16Hivyo msiruhusu matendo yenu mema yakasababisha watu kuwadhihaki. 17Kwa kuwa ufalme wa Mungu si kwa ajili ya chakula na kinywaji, bali ni kwa ajili ya haki, amani, na furaha katika Roho Mtakatifu.

18Kwa kuwa yeye amtumikiaye Kristo kwa jinsi hii amekubalika kwa Mungu na amekubalika kwa watu. 19Kwa hiyo basi, na tufuate mambo ya amani na mambo ambayo humjenga mtu na mwingine.

20Usiharibu kazi ya Mungu kwa sababu ya chakula. Vitu vyote kwa kweli ni safi, lakini ni vibaya kwa mtu yule ambaye hula na kumsababisha yeye kujikwaa. 21Ni vyema kutokula nyama, wala kunywa divai, wala chochote ambacho kwa hicho ndugu yako hukwazwa.

22Hizi imani maalumu ulizo nazo, ziweke kati yako mwenyewe na Mungu. Amebalikiwa yule ambaye hajihukumu mwenyewe katika kile anachokikubali. Aliye na mashaka amehukumiwa ikiwa anakula, kwa sababu haitokani na imani. Na chochote kisichotokana na imani ni dhambi.

23

Copyright information for SwaULB